Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:49

Moise Katumbi ahukumiwa miezi 36 jela


Moise Katumbi, alipokua gavana wa jimbo la Katanga
Moise Katumbi, alipokua gavana wa jimbo la Katanga

Mgombea kiti cha rais Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na mpinzani mkuu wa Rais Joseph Kabila, Moise Katumbi amehukumiwa kifungo cha mieizi 36 jela na kutozwa fini ya dola milioni 6, bila ya kuwepo mahakamani.

Mfanyabiashara huyo tajiri, anayemiliki moja wapo ya klabu mashuhuri ya Afrika TP Mazembe yuko nje ya nchi kwa matibabu, baada ya kufunguliwa mashtaka ya kuwandikisha mamluki kujaribu kupindua serikali ya Kinshasa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:17 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hapo May 20, 2016, Katumbi alisafiri kwenda Afrikia Kusini, siku moja tu baada ya maafisa kutoa hati ya kukamatwa kwake kuhusika na kesi tofauti kuhusiana na kuwaandikisha wamamluki, ili kuipindua serikali. Tuhuma ambazo anazikanusha.

Moise Katumbi akiwapungia mkono wafuasi wake.
Moise Katumbi akiwapungia mkono wafuasi wake.

Mwanasiasa huyo anaeungwa mkono na vyama saba vya upinzani kugombania kiti cha rais amepatikana na hatia na mahakama moja ya Lumbumbashi kwa kununua jengo la makazi kutoka kwa raia mwenye asili ya Ugriki Emmanuel Stoupis kinyume cha sheria.

Katumbi anakanusha tuhuma hizo na mawakili wake wanasema ni njama za serikali kumzuia kugombania kiti cha rais. Kulingana na katiba ya Congo mtu yeyote anaehukumiwa kifungo cha jela kwa uhalifu wowote hawezi tena kugombania kiti cha rais.

XS
SM
MD
LG