Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 13:24

Rais Obama afanya ziara ya kihistoria Hiroshima

Rais Barack Obama wa marekani akiweka shada la maua kwenye Bustani ya Amani ya Hiroshima, maghariobi ya Japan, Ijuama, May 27, 2016.
Rais Barack Obama wa marekani akiweka shada la maua kwenye Bustani ya Amani ya Hiroshima, maghariobi ya Japan, Ijuama, May 27, 2016.

Rais Barack Obama anasema, dunia ina jukumu la pamoja katika kuzuia maafa yaliyotokea Hiroshima kutokea tena, alipokua anatoa heshima zake kwa waathiriwa wa bomu la nuklia lililodondoshwa katika mji huo miongo saba iliyopita.

"Tunasimama hapa kati kati ya mji huo na tunajilazimisha kufikiria na kuwaza hali ilikuaje bomu lilipodondoka.", alisema Rais Obama siku ya Ijumaa akiwa Bustani ya Amani ya Hiroshima.

Rais Barack Obama (kulia) akimpa mkono Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe baada ya kuweka shada la maua.
Rais Barack Obama (kulia) akimpa mkono Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe baada ya kuweka shada la maua.

Obama ni rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kutembelea mji wa Hiroshima tangu shambulio hilo la kumaliza vita vya pili vya dunia.

Akiwa pamoja na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe, Obama alifungua ukurasa mwengine wa kihistoria alipotembelea bustani hiyo ya makumbusho na kukutana na baadhi ya walonusurika na shambuliop la kwanza la nuklia duniani.

Rais Barack Obama (L) amkumbatia Shigeaki Mori mmoja kati ya walonusurika huko Hiroshima
Rais Barack Obama (L) amkumbatia Shigeaki Mori mmoja kati ya walonusurika huko Hiroshima

Takriban watu 140,000 walifariki Hiroshima pale ndege ya kimarekani ilipodondosha bomu Agosti 6, 1945 na wengine 74,000 walifariki siku mbili baadaye katika mlipuko wa pili katika mji wa Nagasaki.

Katika hotuba yake Obama alitoa wito kwa watu kutowasahao waathiriwa wa Hiroshima na kutaka kuwepo na muelekeo mpya kuhusiana na silaha za nuklia.

Mwandishi habari akisimama katika mabaki ya Hiroshima, Japan mwaka1945, wiki chache baada ya shambulio la nuklia
Mwandishi habari akisimama katika mabaki ya Hiroshima, Japan mwaka1945, wiki chache baada ya shambulio la nuklia

XS
SM
MD
LG