Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:26

Rais Hollande: Abdeslam aliyehusika na mashambulizi ya Paris amekamatwa


Polisi wa Ubelgiji wakilinda mtaa ambao Salah Abdeslam alikamatwa
Polisi wa Ubelgiji wakilinda mtaa ambao Salah Abdeslam alikamatwa

Rais Francois Hollande wa Ufaransa amethibitisha kukamatwa kwa muandalizi mkuu wa mashambulizi ya Novemba 13 mwaka jana mjini Paris, wakati wa operesheni maalum ya polisi.

Akizungumza na waandishi habari mjini Brussels pamoja na waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel, Rais Hollande alipongeza vikosi vya usalama vya nchi zao mbili kwa ushirikiano wa kuweza kukamatwa kwa Salah Abdeslam.

Meya wa mji wa Molenbeek karibu na mji mkuu wa Brussels, Francois Shepmans alisema Abdeslam pamoja na mtu mwengine walijeruhiwa wakati polisi walikua wanawasubiri katika nyhumba moja walopata habari kwamba ataweza kujificha.

Maafisa wa usalama wa Ubelgiji waligundua alama za vidole vya kijana huyo mwenye miaka 26 aliyekua anakimbia kutoka nyumba moja wakati wa shambulizi la mapema wiki hii katika mtaa mmoja wa Brussels.

Mshukiwa mwengine wa shambulizi la Paris Mohamed Belkaid mwenye umri wa miaka 35 aliuliwa kwenye shambulizi hilo baada ya vikosi maalum vya usalama vya Ufaransa na Ubelgiji kupata habari za kijasusi kwambe yuko katika nyumba hiyo.

Mashambulio ya Paris yalisababisha vifo vya watu 130 walokua wanapumzika siku ya Ijumaa katika migahawa na ukumbi wa sinema.

XS
SM
MD
LG