Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:45

Karatasi za kupigia kura zawasili Zanzibar


Picha ya vijana wakiimba na kuunga mkono upinzania katika uchaguzi wa urais Zanzibar mwaka 2015.
Picha ya vijana wakiimba na kuunga mkono upinzania katika uchaguzi wa urais Zanzibar mwaka 2015.

Karatasi hizo za kupigia kura zimewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar kwa ndege maalum ya kukodi, zikitokea nchini Afrika Kusini zilikochapishwa na kugharimu kiasi cha shilingi milioni 500.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar Ijumaa imepokea shehena ya karatasi zitakazotumika kwa ajili ya kupigia kura katika uchaguzi mkuu wa marudio unaotarajiwa kufanyika Machi 20 mwaka huu, huku ikiahidi kuwa maandalizi yote ya uchaguzi huo yamekamilika na utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.5.

Uchaguzi wa Zanzibar kufanyika Machi 20
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:08 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mkurugenzi huyo amesema kazi ya kusambaza karatasi hizo katika ofisi za tume za wilaya inatarajiwa kufanyika kuanzia Machi 18, na siku itakayofuata karatasi hizo zitasambazwa katika vituo vya kupigia kura vilivyopo katika visiwa vya Unguja na Pemba ikiwa ni siku moja kabla ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi huo.

Uchaguzi huo wa marudio unafanyika Machi 20, huku baadhi ya vyama vya siasa vikiwa vimetangaza msimamo wa kutoshiriki kutokana na sababu mbalimbali, lakini tume hiyo ya uchaguzi imechapisha picha za wagombea wote walioshiriki katika uchaguzi wa oktoba 25 ambao matokeo yake yalifutwa na Mwenyekiti wa ZEC Alhaj Jecha Salim Jecha.

XS
SM
MD
LG