Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:02

Nancy Reagan, mke wa rais wa zamani wa Marekani afariki


Mke wa rais wa zamani wa Marekani Nancy Reagan akitembelea kaburi la mumewe rais wa zamani Ronald Reagan, miaka 10 baada ya kufariki kwake Simi Valley, California June 5, 2014.
Mke wa rais wa zamani wa Marekani Nancy Reagan akitembelea kaburi la mumewe rais wa zamani Ronald Reagan, miaka 10 baada ya kufariki kwake Simi Valley, California June 5, 2014.

Mke wa rais wa 40 wa Marekani Nancy Reagan, afariki akiwa na umri wa miaka 94 kutokana na matatizo ya moyo.

Mcheza filamu huyo aliyekua mke wa rais wa zamani Ronald Reagan kwa zaidi ya nusu karne, walikua madarakani kuanzia 1981 hadi 1989.

Akiwa mcheza filamu huko Hollywood miaka ya 1940, Ann Francis Robbins - aliyefahamika kama Nancy Davis - alijuana na mumewe Ronald Reagan aliyekua mcheza filamu pia, na kuoana 1952.

Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan na mkewe Nancy
Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan na mkewe Nancy

Mumewake alikua gavana wa jimbo kuu la California kuanzia 1967 hadi 1975. Aligombania kiti cha rais kwa mara ya kwanza na kushinmdwa mwaka 1976. Hapo tena kugombania kwa mara ya pili 1981.

Kama mke wa rais aliongoza kampeni ya kupambana na dawa za kulevya "Just Say No to Drugs", na kuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la kitaifa la kupambana na dawa za kulevya wakati huo.

Nancy alikua mshauri mkuu wa mumewe na alikosolewa kwa matumizi makubwa katika White House. Atazikwa kando ya kaburi ya mumewe katika Maktaba ya Rais Ronald Reagan huko Sim valley, California

Nancy anawaacha nyuma watoto wawili, Patti Davis na Ron Reagan.

Mke wa rais wa zamani Nancy Reagan afariki
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:20 0:00

XS
SM
MD
LG