Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:40

Balozi wa Marekani nchini Kenya azuru Mombasa


Balozi wa Marekani nchini kenya wapili kulia Robert F. Godec.
Balozi wa Marekani nchini kenya wapili kulia Robert F. Godec.

Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Mombasa balozi Godec amesema kuwa ushirikiano mzuri kati ya Marekani na Kenya katika kukabiliana na ugaidi umezaa matunda huku akiwarai mabalozi wengine kuwashauri raiya wao kuzuru eneo hilo.

Balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec amepongeza ushirikiano uliopo kati ya serikali kuu ya Kenya na zile ya kaunti katika eneo la Pwani ya Kenya kuimarisha usalama na kufanya eneo la Pwani kuwa salama kwa watalii.

Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Mombasa Godec amesema kuwa ushirikiano mzuri kati ya Marekani na Kenya katika kukabiliana na ugaidi umezaa matunda huku akiwarai mabalozi wengine kuwashauri raiya wao kuzuru eneo hilo.

Balozi Godec azuru Mombasa
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:54 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Huku hayo yakijiri Viongozi mbali mbali katika eneo la Pwani ya Kenya wamewahimizaviongozi wa kisiasa kupungua cheche za siasa ambazo zinatishia kuharibu mafanikio ambayo yamepatikana katika eneo hilo haswa katika secta ya utalii.

Waziri wa utalii Najib Balala amewataka wanasiasa kupunguza malumbano hayo ikiwa wanataka kunufaika na shilingi bilioni 5.2 ambazo serikali imewekeza kuimarisha sekta ya utalii.

Balala amesema kuwa kwa sasa anaendelea na juhudi za kuilainisha sekta nzima ya utalii na ikiwa wanasiasa wataendelea na mkondo waliochukua hivi karibuni utatishia wawekezaji.

Usemi huu pia umesisitizwa na viongozi wa kidini katika eneo la Pwani wakiongozwa na katibu mku wa baraza la maimamu na wahubiri nchini CIPK Momhamed Khalifa ambaye amewataka viongozi kushindana kuwapa wakenya maendeleo badala ya cheche za maneno.

XS
SM
MD
LG