Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:44

Ethiopia Inakabiliwa na Ukame Mbaya


Ethiopia inakabiliwa na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 50, huku shirika la Save the Children likitoa wito wa haraka wa msaada wa chakula.

Shirika hilo limesema msaada huo utakuwa ni suluhisho la mda tu, na viongozi wa dunia wanaokutana mjini Paris lazima wachukuea hatua juu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Serikali ya Ethiopia inasema watu millioni 10 na laki moja watakabiliwa na upungufu wa mkubwa wa chakula mwaka 2016, na zaidi ya nusu ya hao ni watoto.

Kadhalika kuna watoto takriban laki 4 walio katika hatari ya kukumbwa na utapia mlo mkubwa, hali ambayo inaweza kusababisha kudumaa kwa ukuwaji na matatizo ya akili.

John Graham, mkurugenzi wa shirika la Save the Children nchini Ethiopia, amesema mzozo wa mwaka huu ni matokeo ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Ukame mbaya unahusishwa na mfumo wa hali ya hewa ujulikanao kama El Nino umeharibu misimu miwili mikuu ya mvua nchini humo mwaka huu na kutokana na hilo mavuno yajayo hayatarajiwi kuja hadi mwezi Juni mwakani.

Idara ya Umoja wa Mataifa ya Chakula na Kilimo (FAO) inakadiria kuwa takriban aslimia 80 ya Waethiopia wanafanya kazi katika sekta ya kilimo, na wengi wao ni wakulima wa wadogo wadogo ambao wanategemea mvua kwa kilimo.

Hiyo ndio sababu taifa hilo linakumbwa na mizozo ya chakula mara kwa mara na wakulima wanakosa njia na elimu ya kukabiliana na changamoto za hali ya hewa.

Shirika la Save the Children linaomba msaada wa takriban dola millioni 100 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa lakini limesema mwaka huu majibu yamekuwa ya pole pole mno.

XS
SM
MD
LG