Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 18:52

Obama Atoa Wito wa Kutanzua Matatizo ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa


Viongozi wa dunia wakipiga picha kabla ya kuanza mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa Paris COP21.
Viongozi wa dunia wakipiga picha kabla ya kuanza mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa Paris COP21.

Rais Barack Obama wa Marekanio amewataka viongozi wa dunia kuungana nae katika juhudi za kutanzua matatizo yanayosababisha mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa huko Paris Ufaransa, unaohudhuriwa na viongozi kutoka zaidi ya mataifa 150, Rais Obama amewahimiza viongozi wenzake kuungana nae kuchukua hatua zinazostahiki ili kutanzua matatizo ya mabadiliko ya hali ya hewa ili kuiokoa dunia yetu.

Amesema viongozi wanaohudhuria mkutanop wanakabiliwa na hali ya dharura kupunguza uchaguzi wa hewa kwa gesi za sumu na kuzuia kuongezeka kwa joto duniani.

"Jukumu letu hapa Paris ni kutumia mafanikio yaliyopatikana hadi sasa na kuhakikisha yanakuwa endelevu na kufikia makubaliano kwaajili ya maendeleo ya binadamu. Hatutaki suluhisho la viraka bali tunahitaji mkakati wa muda mrefu ," alisema Obama.

Viongozi wa dunia wanabidi baada ya wiki mbili kufikia makubaliano thabiti ya kuzia kuongezeka joto, kukubaliana mpango wa kusaidia mataifa yanayoendelea yanayokabiliwa na athari kubwa zaidi, pamoja na viwango kila nchi inabidi kufikia katika kupunguza uchafuzi wa mazingira.

XS
SM
MD
LG