Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:25

Burundi yaishutumu Ubelgiji kufadhili makundi ya upinzani.


Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunzinza.

Chama tawala nchini Burundi Alhamisi kimetoa matamshi makali dhidi ya nchi ya ubeligiji iliyotawala nchi hiyo wakati wa ukoloni.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:39 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mbali na kutuhumu nchi hiyo kufadhili makundi ya yanayotaka kuipindua serikali ya chama hicho, wakati huu ambapo Burundi inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa, chama cha CNDD FDD kinalaani pia hatua ya nchi hiyo ya Ubelgiji kuwataka raia wake waishio Burundi kurejea makwao kabla hali ya usalama haijawa mbaya zaidi.

Tamko hilo lilitolewa kwenye radio ya kitaifa nchini Burundi katika lugha nne, “chama kimeomba wananchi kuungana kwa pamoja ili waweze kuishitaki Ubelgiji katika mahakama za ndani ya nchi na kimataifa kwa ajili ya maovu waliyotenda” alisema Jenerali Ndabizabi.

Aliongeza chama hicho kinafuatilia kwa karibu masuala kadhaa na kuona wafaransa wakoloni wa Senegal, Ivory Coast na nchi nyinginezo ni wakili mzuri wa makoloni hayo katika mataifa mengine lakini akadai kwamba kitu cha ajabu ni kwamba Ubelgiji daima imejishughulisha kutaka kupindua serikali ya nchi iliyotawala kwa mfano Burundi.

XS
SM
MD
LG