Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 12:27

Ubadhirifu Katika County Nyingi Kenya


Kikao cha bunge la Kenya
Kikao cha bunge la Kenya

Serikali ya Kenya inakumbwa na msukosuko wa rushwa na utumiaji mbaya wa fedha kutokana na upande mmoja ripoti juu ya matumizi katika county na shinikizo kutoka upinzani kumtaka rais uhuru Kenyatta kuchukua hatua za kumfukuza waziri wa ugatuzi na maendeleo bi anne waiguru.

Seneta James Mungai wa Nakuru County
Seneta James Mungai wa Nakuru County

Akizungumza na Sauti ya Amerika Seneta wa Nakuru James Mungai, ambae ni mwanachama wa kamati ya fedha na bajeti ya Baraza la Senet, la Bunge anasema tatizo kubwa ni kwamba huu ni mfumo mpya wa utawala na magavana wengi hawajafahamu namna ya kutumia fedha nyingi wanazopokea.

“Shida moja ni kwamba kwa wakati huu auditor general ndiyop anatowa ripoti ya matumizi ya 2013 na 2014, kwa hivyo inachukua muda mrefu sana bila sisi kujua ni shida gani zilizopo katika macounty.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bw Mungai anasema kwa wakati huu tume imeanza kuwaita magavana ili wajieleze namna walivyotumia fedha za umaa.

“Mambo tunayofanya hivi sasa ni kuwaita magavana na kuwasikiliza moja kwa moja wale walokwishatajwa kwamba county zao kuna shida. Wengi wao wanashindwa kufafanua hali ya mambo yalivyo. Kwa hivyo inaonekana kwamba fedha zimeshapotea, na hivyo inabidi wengi wao kuwafikisha mbele ya kortini”.

Anne Waiguru Waziri wa Ugatuzi na Mipango
Anne Waiguru Waziri wa Ugatuzi na Mipango

Kwa upande mwengine waziri wa ugatuzi na mipango Anne Waiguru alijifikisha mbele ya tume ya maadili na kupambana na rushwa siku ya Jumanne ili kuzungumzia tuhuma dhidi ubadhirifu na rushwa katika wizara yake. Tuihuma kuu ni ubadhirifu katika idara ya mipango, na idara ya taifa ya vijana NYS, ambapo inadaiwa zaidi ya shilingi milioni 791 za Kenya zimepotwa.

XS
SM
MD
LG