Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:31

Umoja wa Mataifa Unaongoza Mazungumzo Zanzibar


Mt6u anapiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, October 25, 2015.
Mt6u anapiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam, October 25, 2015.

Juhudi za kutafuta suluhisho kwa mzozo wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar unaendelea kwa kuwepo na mazungumzo kati ya wapatanishi wa kimataifa na wanasiasa wa Zanzibar.

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki Moon pamoja na wawalkilishi wengine wa jumuia za kikanda wanaendelea na juuhudi za kutafuta njia za kutanzua mzozo ulosababishwa na kufutiliwa mbali ucahguzi mkuu wa Zanzibar na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jecha Salim Jecha, tarehe 28 Oktoba

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Hadi hivi sasa hakuna taarifa rasmi iliyotolewa juu ya juhudi hizo , hata hivyo kiongozi wa upinzani Maalim Seif Shariff Hamad alilalamika mwishoni mwa wiki kwamba anashindwa kuwasiliana na Rais Jakaya Kikwete ili kuzungumzia mzozo huo.

Jabir Idriss mhariri wa gazeti la Mwanahalisi anasema, "kwa mujibu wa habari zilizopatikana jioni hii Maalim Seif amemuandikia Rais Jakaya Kikwete, barua akimuomba akutane nae ili kuzungumzia hali ya kisiasa ya Zanzibar."

Kiongozi huyo wa upinzani anamatumaini pia kuzungumza na mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania Jenrali Davis Mwamunyange, kuzungumzia hali ya usalama visiwani humo.

XS
SM
MD
LG