Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:06

Waasi wa Sudan Kusini watia saini makubaliano ya amani.


Kiongozi wa upinzani Sudan Kusini Riek Machar akizungumza na waandishi wa habari, Nairobi, Kenya, Julai 8, 2015.
Kiongozi wa upinzani Sudan Kusini Riek Machar akizungumza na waandishi wa habari, Nairobi, Kenya, Julai 8, 2015.

Waasi wa Sudan Kusini walitia saini makubaliano Jumatatu ili kuhitimisha utekelezaji wa mipango ya usalama ambayo ilikuwa sehemu ya makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwezi wa Agosti. Hata hivyo mapigano yameendelea licha ya kuwepo na makubaliano ya kusitisha mapigano, lakini matukio haya mapya yanazipa pande zote matumaini.

Ujumbe wa jeshi la waasi wa Sudan Kusini walitia saini waraka zinazoelezea hatua za makubaliano ya usalama hapo Jumatatu. Ujumbe wa serikali na kundi la viongozi wa zamani wa kisiasa, kadhalika wafungwa, walitia saini makubaliano hapo Septemba, lakini waasi walikuwa wamekataa.

Jenerali Taban Deng Gai, anasema waasi walichelewesha kutia saini kwa sababu walikuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya wanajeshi katika mji mkuu wa Juba.

Mazungumzo yataendelea kuamuwa juu ya vipengele kuhusu kugawana kwa vikosi. Jumuiya ya ushirikiano wa serikali za Africa Mashariki na pembe ya Afrika , IGAD, ambayo inaongoza juhudi za upatanishi, ina matumaini kwa maendeleo zaidi kufanyika baada ya kutiwa saini makubaliano hayo hiyo jana.

Naibu waziri wa masuala ya nchi za nje, wa Sudan Kusini Peter Bashir, anaita kutiwa saini kuwa ni ufumbuzi muhimu katika mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea kwa miezi 22.

"Hati hii ya melezo kulingana na makubaliano , inatarajiwa kuwa ndiyo usimamiaji wa makubaliano ya kudumu ya kusitisha mapigano na mipango ya mpito wa usalama, ambao ni muhimu kwa utekelezaji wa vipengele venginevyo.” alisema Bashir.

Mzozo wa kisiasa baina ya rais Salva Kiir na makamu rais wake wa zamani uligeuka na kuwa ghasia hapo mwezi December mwaka 2013. Mzozo umewasababisha mamillioni ya watu kupoteza makazi na kuhitaji msaada wa dharura.

Umoja mataifa umeonya mwezi huu kuwa takriban watu millioni 4 huko Sudan Kusini wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula, ikiwa ni pamoja na maelfu ya watu walio ukingoni mwa kukabiliwa na njaa katika jimbo lilokabiliwa na vita la Unity.

Makubaliano kadhaa yametiwa saini tangu Januari 2014, lakini hamna ulioleta amani.



XS
SM
MD
LG