Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 12:36

Hatimaye Watanzania wapiga kura leo


Mmmoja wa wapiga kufa nchini tanzania
Mmmoja wa wapiga kufa nchini tanzania

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandishi wetu walioko mikoa kadhaa nchini humo , wanasema hali inaonesha kuwa shwari licha ya kuwepo kasoro chache kama masundu ya kura kuchelewa katika vituo vya kupigia kura.

Watanzania wanapiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais wa awamu ya tano atakayerithi nafasi ya rais Jakaya Mrisho Kikwete ambaye anaondoka madarakani baada ya kutumikia taifa hilo kwa mihula miwili yaani miaka 10

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa waandishi wetu walioko mikoa kadhaa nchini humo , wanasema hali inaonesha kuwa shwari licha ya kuwepo kasoro chache kama masundu ya kura kuchelewa katika vituo vya kupigia kura.

Kampeni za awamu hii zilikuwa nzito na moto hasa kutokana na kwamba upande wa upinzani uliunga nguvu kwa kuungana na kusimamisha mgombea mmjoa atayepeperusha benderea ya Ukawa.

Kwa upande wa CCm chama tawala nchini Tanzania kilichokuwepo madarakani kwa zaidi ya miaka 50 nacho kimefanya juhudi kubwa katika kujitetea chini ya mgombea John Pombe Magufuli.

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi Jumapili na vinatarajiwa kufungwa saa kumi za jioni.

Waangalizi wa kimataifa zaidi ya 40 wakiongozwa na aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan wako nchini kwa ajili ya kufuatilia uchaguzi wa Tanzania.

XS
SM
MD
LG