Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:37

Waziri wa mambo ya ndani wa Uganda afariki


Jenrali Aronda Nyakairima, kamanda wa jeshi akizungumza na waandishi habari
Jenrali Aronda Nyakairima, kamanda wa jeshi akizungumza na waandishi habari

Waziri wa mambo ya ndani wa Uganda, Jenerali Aronda Nyakairima afariki ghafla asubuhi Jumamosi akiwa njiani anarudi nyumbani kutoka ziara rasmi ya Korea Kusini.

Taarifa ya Waziri Mkuu Ruhakana Rugunda inaeleza kwamba Jenerali Nyakairima, aliyekua na umri wa miaka 56, alifariki aliposimama Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kubadilisha ndege kuelekea Kampala.

Taarifa inaeleza kwamba Nyakairima aliyepata mafunzo yake Marekani akiwa afisa kijana, "alikua mtumishi aliyejitolewa kuwatumikia waganda na kifo chake ni pigo kubwa kwa taifa."

Tume maalum ya madaktari imeshapelekwa Dubai kuchunguza sababu za kifo hicho na kutayarisha mipango ya kurudisha mwili wake nyumbani.

Jenerali alitumika kama waziri wa mambo ya ndani tangu 2013. Kabla ya hapo alikua mkuu wa majeshi ya Uganda na anasifiwa kwa kusiadia kumondowa kiongozi wa waasi Joseph Kony kutoka Uganda.

Kifo chake kimewashtusha wengi Uganda hasa kwa vile Nyakairima alikua moja wapo ya maafisa wakuu watatu walotajwa mwaka 2013 katika barua ya jenerali wa Uganda aliyeasi David Sejusa, kwamba wako tayari kuhatarisha maisha yao kwa sababu ya kupinga kupanda juu kisiasa kwa mtoto wa Rais Yoweri Museveni.

XS
SM
MD
LG