Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 12:11

Wahamiaji wasiopungua 200 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Libya.


Coffin of victims are seen in an hangar of Lampedusa airport on October 5, 2013 after a boat with migrants sank killing more than hundred people. Italy mourned today the 300 African asylum-seekers feared dead in the worst ever Mediterranean refugee disast
Coffin of victims are seen in an hangar of Lampedusa airport on October 5, 2013 after a boat with migrants sank killing more than hundred people. Italy mourned today the 300 African asylum-seekers feared dead in the worst ever Mediterranean refugee disast

Mzozo wa Uhamiaji kuelekea Ulaya unazidi kuwa hatari na kutia wasi wasi kutokana na idadi ya watu wanaofariki wakijaribu kutafuta maisha bora kutoka Afrika Mashariki ya Kati na Afia.

Mnamo wiki hii zaidi ya wahamiaji 400 wameshafariki. Siku ya Ijuma maafisa wa usalama baharini huko Libya wamesema wanahofu kwamba watu wapatao 200 huwenda wamekufa baada ya boti iliyojaza wahamiaji kuzama nje ya pwani ya Libya, lakini idadi kamili ya watu waliokuwemo ndani ya boti bado haijulikani.

Maafisa wanasema walinzi wa pwani wa Libya waliwaokoa watu 200 wengine kutoka kwenye boti hiyo iliyozama kwenye ufukwe wa mji wa Zuwara nchini Libya, Alhamisi usiku. Maafisa wa usalama wamesema wahamiaji wengi waliokuwa ndani ya boti walikuwa kutoka nchi za kusini mwa jangwa la Sahara barani Afrika, Pakistan, Syria, Morocco na Bangladesh.

Mhamiaji mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba boti hiyo ilikuwa katika hali mbaya. Alisema njia ya kwenda Libya ilikuwa ikiitwa njia ya kifo lakini sasa inaitwa kaburi la bahari ya Mediteranean.

Maafisa wa Austria wanasema wamewakamata watu watatu waliohusishwa na miili 71 ya wahamiaji iliyogundulika katika lori kwenye barabara moja kuu ya Austria karibu na mpaka na Hungary. maafisa wamesema mapema leo kwamba watu wawili kati ya hao waliokamatwa ni raia wa Bulgaria, wakati mtu wa tatu ana uraia wa Hungary.

Polisi wa Austria pia wanasema makadirio yao ya awali ya idadi ya watu waliokuwa ndani ya lori hilo yalikuwa chini. Hapo jana walitangaza waathirika 20 hadi 50 wamegundulika, na hii leo idadi ya waathirika imeongezeka kufikia 71.

Waathirika 50 wanaume, wanane wanawake na watoto wane wanaaminika walifariki kutokana na hewa chafu ndani ya lori hiyo ya kuhifadhi vitu baridi.

Maafisa wanasema watu wasiopungua 2,400 wamefariki dunia wakijaribu kuelekea Ulaya kwa boti mwaka huu kiwango kilicho kikubwa kuliko wakati kama huu mwaka jana.

XS
SM
MD
LG