Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 02:03

Lowassa Achukuwa Fomu ya Urais kwa Maandamano Makubwa


CHADEMA and Edward Ngoyai Lowassa and Juma Duni Hajji
CHADEMA and Edward Ngoyai Lowassa and Juma Duni Hajji

Uchaguzi mkuu wa mwaka huu nchini Tanzania huenda ukashuhudia msisimko wa aina yake ambao haujawahi kutokea katika uchaguzi wowote uliopita kutokana na ushindani unaoonekana baina ya chama tawala na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.

Ushuhuda wa aina ya ushindani katika uchaguzi mkuu mwaka huu umeonekana leo jijini Dar es salaam ambapo karibu shughuli zote zilisimama kwa muda baada ya mamia ya wapenzi, wanachama na mashabiki wa vyama vinavyounda katiba ya waanchi UKAWA kuwasindikiza mgombea urais na mgombea mwenza kupitia umoja huo Edward Lowassa na Juma Duni Haji kwa ajili ya kuchukua fomu tume ya taifa ya uchaguzi NEC.

Mitaa ya jiji la Dar es salaam kuanzia makao makuu ya Chama Cha Wananchi CUF ambapo msafara wa mgombea ulianzia kupitia buguruni ilala mpaka kufika ofisi ya tume ya taifa ya uchaguzi ilijaa watu wa aina mbalimbai na kufanya polisi kufanya kazi ya ziada kuimarisha ulinzi lakini bila kuzuia maandamano hayo makubwa.

Baada ya kukabidhiwa fomu hizo tume ya taifa ya uchaguzi msafara wa wagombea hao ulieleka makao makuu ya CHADEMA kinondoni ambapo ndipo baadhi ya viongozi wa UKAWA akiwemo Maalim Seif Shariff Hamad, katibu mkuu wa Taifa wa CUF taifa ambapo alizungumzia muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Uchaguzi mkuu wa mwaka huu nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu nchini kote kwa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais

XS
SM
MD
LG