Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 07:20

Kenya yasema kuna uhusiano biashara ya Pembe na MRC


Mafisa wa idara ya wanyamapori Kenya wakionesha pembe za kifaru
Mafisa wa idara ya wanyamapori Kenya wakionesha pembe za kifaru

Maafisa wa usalama wa Kenya wanasema wameweza kuunganisha uhusiano uliopo kati ya bishara haramu ya pembe za ndovu huko Asia na kufadhiliwa kwa kundi la pwani linalotaka kujitenga la MRC.

Taarifa kutoka kwa waziri wa mambo ya ndani Joseph Nkaissery inaeleza kwamba, watu 14 wamekamatwa kuhusiana na shehena ya pembe za ndovu zilizosafirishwa hadi Thailand, na fedha kulipwa kundi linalopigania kujitenga kwa pwani la Mombasa Republican Council, MRC.

Wakuu wa kundi hilo lililopigwa marufuku, wanasisitiza kwamba lengo lao ni kutetea haki na uhuru wa waislamu wa Kenya. Imekanusha mara kwa mara kuhusika na mlolongo wa mashambulizi katika eneo la pwani la taifa hilo.

XS
SM
MD
LG