Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 10:14

Maafisa wa vyeo vya juu wa FIFA wakamatwa kwa ajili ya rushwa


Mbele ya ukumbi wa Hallenstadion, ambako mkutano mkuu ujao wa 65th FIFA utafanyika mjini Zurich, Uswisi, May 26, 2015.
Mbele ya ukumbi wa Hallenstadion, ambako mkutano mkuu ujao wa 65th FIFA utafanyika mjini Zurich, Uswisi, May 26, 2015.

Maafisa wa usalama wa Uswisi wanasema wanawashikilia maafisa kadhaa wa vyeo vya juu ya Shirikisho la Kimataifa la Kandanda FIFA kwa tuhuma za ulaji rushwa na kupokea hongo na baadhi yao watasafirishwa hadi Marekani.

Gazeti la New York Times likiripoti juu ya tukio hilo linaeleza kwamba maafisa wa usalama walova mavazi ya kiraia waliwasili katika hoteli ya Baur au Lac alfajiri Jumatano, na kuchukua ufunguo wa baadhi ya vyumba vya maafisa hao na kuelekea katika vyumba vyao.

New York Times likiwanukua maafisa wa usalama wa Uswisi wasotaka kutajwa, inaripoti kwamba serikali kuu ya Marekani inawashitaki maafisa hao kwa ubadhirifu wa mali, kuhalalisha fedha zilziopatikana kwa njia zisizo halali katika kipindi cha miaka 20 hadi leo.

Maafisa hao walokamatwa wamefika Zurich kuhudhuria mkutano mkuu wa FIFA ambao unatazamiwa kumchagua tena Sepp Blatter ambae anakabiliwa na upinzani kutoka kwa mwana mfalme wa jordan Ali Bin Al Hussein hapo Ijuma.

XS
SM
MD
LG