Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 19:09

Waziri wa mambo ya ndani Burundi akanusha madai ya mapinduzi.


Jumuiya ya Kimataifa yalaani mapinduzi Burundi
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:14 0:00

Afisa wa juu wa Burundi anakanusha habari ya kupinduliwa kwa rais wa nchi hiyo na Jenerali muasi.

Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Edourd Nduwimana ameiambia Sauti ya Amerika kwamba wanajeshi wanaomuunga mkono Rais Pierre Nkurunzinza bado yanadhibiti nchi ikiwa ni pamoja na ikulu ya rais, radio na televisheni ya taifa na uwanja wa ndege katika mji mkuu Bujumbura.

Amesema rais amesharudi Burundi kutoka Tanzania ambako alihudhuria mkutano wa viongozi wa kikanda juu ya nchini mwake siku ya Jumatano, ingawa hakusema mahala alipo Bw.Nkurunzinza.

Mkutano wa Jumatano huko Dar es Salaam uliitishwa na Jumuia ya afrika Mashariki kujadili mzozo wa Burundi, kutokana na hofu kwamba taifa hilo huwenda likatumbukia tena katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

White house imetoa wito wa kukomeshwa mara moja ghasia na pande zote kuweka silaha chini. Msemaji wa White House Josh Earnest alieleza pia uungaji mkono juhudi zinazoendelea za viongozi wa kanda kurudisha Amani na umoja katika nchi hiyo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani inaeleza kwamba wanadiplomasia wa Marekani walizungumza na washauri wakuu wa rais mapema Jumatano. Lakini msemaji huyo amesema mazungumzo hayo huenda yalifanyika kabla ya madai ya mapinduzi kutolewa.

Mapema Jenerali Godefroid Niyombare alitangaza kupitia vituo vya radio binafsi vya Burundi kwamba ras amepinduliwa na kusema kwamba ataunda kamati ya “kudumisha Amani na Umoja wa Kitaifa.”

Profesa wa masuala ya sheria kutoka Ubelgiji Filip Reyntjens, mtaalamu wa masuala ya kanda ya Maziwa Makuu, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba Niyombare, akiwa mkuu wa usalama wa nchi alimwonya rais katika taarifa ndefu mapema mwaka huu kutogombania tena awamu ya tatu.

Mwenyekiti wa Tume ya Afrika AU, Bi. Nkosazana Dlamini Zuma amelaanli jaribiop la mapinduzi nchini Burundi na kutoa wito wa kurudi kwa utawala wa kikatiba.

Ufaransa vile vile imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuitisha mkutano wa dharura juu ya Burundi.

XS
SM
MD
LG