Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:39

Baraza la Usalama lasikitishwa na Sudan Kusini


Wanajeshi watoto wa Sudan Kusini
Wanajeshi watoto wa Sudan Kusini

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelezea kusikitishwa kwake kutokana na rais wa Sudan Kusini, na kiongozi wa waasi Riek Machar kusindwa kufikia makubaliano ya amani.

Katika taarifa iliyotolewa na baraza hilo Jumanne, kwa mara nyingine tena imetishia vikwazo dhidi ya maafisa wa juu ambao inahisi wanawajibika na vitendo ama sera ambazo zitatishia amani, usalama, ama uthabiti ndani ya Sudan Kusini.

Mapigano katika taifa hilo tajiri la mafuta la Afrika Mashariki, yamesababisha vifo vya maelfu ya watu na kukosesha makazi zaidi ya watu milioni mbili.

Marekani, na Umoja wa Ulaya tayarri zimeshawawekea vikwazo makomanda wqa pande zote mbili.

XS
SM
MD
LG