Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:51

Misri, Ethiopia na Sudan zakubaliana matumizi ya mto Nile


Sehemu ya mto Nile nchini Misri.
Sehemu ya mto Nile nchini Misri.

Misri, Ethiopia na Sudan zimeweka saini mpango wa kutumia maji ya mto Nile, kwa pamoja.

Makubaliano yanaiwezesha Ethiopia, kuendelea na ujenzi wake wa bwawa kubwa kwenye mto huo.

Waziri wa maji wa Ethiopia, Akenayehu Tegenu, amesema hayo Jumatatu, wakati akizungumza na Sauti ya Amerika.

Tegenu, amesema kwamba nchi hizo zimekubaliana maji kutoka mto Nile, ni muhimu kwa mataifa yote matatu kwa matumizi ya binadamu na maendeleo.

Amesema iliwachukuwa maafisa kutoka nchi tatu miezi kadhaa kufikia maafikiano ambayo yanajumuisha taratibu saba ikiwemo kuto sababisha matatizo kwa nchi zao na kutatua migongano kwa kupitia njia za amani.

Tazatibu za kina zitafanyiwa kazi katika makubaliano ya baadaye.

XS
SM
MD
LG