Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:30

Upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania bado una changamoto.


Waandamanaji jijini Dar es Salaam wakidai mageuzi ya katiba kabla ya uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania.
Waandamanaji jijini Dar es Salaam wakidai mageuzi ya katiba kabla ya uchaguzi mkuu ujao nchini Tanzania.

Suala la upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania bado linapita katika kipindi kigumu wakati huu ambapo wananchi wanatarajiwa kupiga kura ya maoni ya ama kuikubali au kuikataa katiba inayopendekezwa ifikapo April 30 mwaka huu.

Wakati viongozi wa umoja wa katiba ya wananchi- UKAWA unaoundwa na vyama vinne vya upinzani vya CUF, NCCR MAGEUZI, NLD na CHADEMA wakiwa wameshatoa msimamo wa kutaka wafuasi wao kususia kabisa zoezi la kura ya maoni kwa katiba inayopendekezwa ambayo itapigiwa kura Aprili 30 mwaka huu, kumeibuka pia hoja nyingine nzito kutoka kwa jumuiya ya Kikristo Tanzania( CCT ) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC).

Jumuiya hizo kubwa za Kikristo nchini zimetoa waraka ulioitwa wa kichungaji wa kuwataka waumini wao kujiandikisha kupiga kura ya maoni , lakini hata hivyo ikiwataka waipige kura ya HAPANA katiba inayopendekezwa.

Msimamo huo umepokelewa kwa hisia tofauti, na watu wa kada mbalimbali nchini Tanzania akiwemo askofu mkuu wa jimbo kuu la Dar es salaam Muadhama Kardinali Polycap Pengo ambaye amepingana na waraka huo akitaka watanzania waachiwe kuamua hatma yao katika katiba inayopendekezwa.

Siku ya Jumatatu jijini Dar es salaam waziri wa sheria na katiba wa Tanzania Asha Rose Migiro akiwa kwenye shughuli ya ugawaji wa katiba inayopendekezwa kwa taasisi mbalimbali amejikuta akikumbana na maswali mbalimbali kuhusiana na msimamo wa wadau juu ya katiba ikiwemo hili la waraka wa kichungaji wa kura ya hapana kwa katiba inayopendekezwa.

Waziri Migiro pia amepuuzia madai kwamba watanzania hawatakuwa tayari kupiga kura ya maoni ifikapo Aprili 30 mwaka huu kutokana na madai kwamba uandikishaji wapiga kura kwa mfumo mpya wa BVR bado ni wa kusuasua.

Waziri wa katiba na sheria Dk. Migiro pia amesema ugawaji wa nakala za katiba pendekezwa katika mikoa yote umekamilika na zoezi hilo la Jumatatu ni awamu ya pili ambapo jumla ya nakala millioni 2 zimegawiwa Tanzania nzima.

XS
SM
MD
LG