Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:26

Wanajeshi wa Afrika Mashariki wapewa mafunzo kupambana na ugaidi.


Jenerali William Ward, kamanda wa AFRICOM commander.
Jenerali William Ward, kamanda wa AFRICOM commander.

Wanajeshi wa Marekani wanatoa mafunzo ya kijeshi kwa wanajshi kutoka nchi sita za Afrika mashariki na Uholanzi katika jitihada za kuimarisha ulinzi wa raia kutokana na vitisho vya makundi ya kigaidi kama vile vitisho vya Al-shabab.

Mafunzo hayo yanalenga kuimarisha mbinu na jitihada za wanajeshi kushirikiana na kupambana na ugaidi.

Mafunzo hayo ya wiki mbili yanafanyika katika kambi ya kijeshi ya Gadafi mjini Jinja Mashariki mwa Uganda.

Pamoja na mafunzo hayo ya kupambana na ugaidi serikali ya Marekani imeipa Uganda ndege mbili za kivita aina ya Cessna 3208 Bay.

Nchi hizo za Afrika mashariki ni pamoja na Uganda, Kenya , Burundi, Djibouti, Tanzania na Rwanda .

XS
SM
MD
LG