Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:51

Obama asema dunia haipigani na Uislam.


Rais Barack Obama akizungumza huko White House katika mkutano maalum uliolenga kupambana na itikadi za msimamo mkali, Feb. 18, 2015 huko Washington.
Rais Barack Obama akizungumza huko White House katika mkutano maalum uliolenga kupambana na itikadi za msimamo mkali, Feb. 18, 2015 huko Washington.

Rais wa Marekani Barack Obama amewasihi viongozi wa makundi ya kiraia na kidini duniani kote kuungana katika mapambano dhidi ya kile alichokiita “ahadi za uongo za wenye msimamo mkali” na kupinga dhana kwamba magaidi wanawakilisha Uislam.

Katika mkutano Jumatano jijini Washington uliolenga kupambana na itikadi za msimamo mkali, bw. Obama alisema wenye msimamo mkali , “wanajaribu kujionyesha kama viongozi wa kidini na mashujaa wa kidini.” Obama alisema watu hao si viongozi wa kidini, ni magaidi.

Rais huyo wa Marekani aliendelea kusema “hatuna vita na Uislam, tuko vitani na watu waliokufuru Uislam.”

Aliuwambia mkutano huo wa siku tatu kwamba pambano dhidi ya watu wenye msimamo mkali halitaweza kufanikiwa kwa nguvu za kijeshi pekee. Alitoa mwito wa moja kwa moja kwa viongozi wa Kiislam kupinga wale wenye msimamo mkali na kuwataka wazungumze kwa sauti kuondoa dhana kwamba kuna nchi ambazo zinapinga Uislam.

XS
SM
MD
LG