Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:06

Washukiwa wa ugaidi Ufaransa wauliwa


Askari wa Ufaransa katika juhudi za kupambana na washukiwa wa ugaidi
Askari wa Ufaransa katika juhudi za kupambana na washukiwa wa ugaidi

Wakuu wa usalama wa Ufaransa wanaeleza kwamba washukiwa wawili kwenye shambulizi katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo wameuwawa na mateka wao kuachiliwa wakati wa uvamizi ulkofanywa na maafisa wa usalama kaskazini mashariki ya Paris.

Kwenye uvamizi mwingine siku ya Ijuma, mshambulizi aliekuwa amewashika mateka watu kadhaa ameuwawa kwenye duka la chakula la kiyahudi lakini polisi wamesema kwamba mateka watatu wamekufa pia katika operesheni hiyo.

Milipuko na milio ya bunduki ilisikika kati kati ya Paris na mtaa wa viwanda wa kaskazini wa Dammartin–en–Goele wakati polisi na wanajeshi walipoingia kwa wakati mmoja adhuhuri ya leo.

Ndugu wawili Cherif na Said Kouachi ambao walitajawa kama washukiwa wakuu katika shambulizi baya la juma hili kwenye ofisi ya gazeti la vichekesho mjini Paris walitoka ndani ya ghala ambapo walikuwa wamejificha na kuanza kuwafyetulia risasi polisi walipokaribia. Waliuliwa wakati polisi waliokuwa wengi walipo wafitulia risasi.

Na wakati wa shambulio mjini Paris kwenye duka la vyakula, maafisa wa usalama walivamia duka karibu na mtaa wa Porte de Vincennes mahala ambapo wayahudi wengi wanapoishi.

Walimuua mtu aliekuwa na bunduki amabae alikuwa ameingia ndani ya duka hilo na kuwashika mateka wanunuzi na wafanyakazi. Maafisa wa usalama wamesema kulikuwa na mateka angalao watano na wane wao waliuwawa na haijabainika nani aliyewauwa na wakati walipouliwa.

XS
SM
MD
LG