Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:01

Tanzania na tuhuma za rushwa: Kashfa ya Mali asili.


Tembo wa Tanzania katika hifadhi ya Tarangire ambao wako hatarini kutoweka.
Tembo wa Tanzania katika hifadhi ya Tarangire ambao wako hatarini kutoweka.

Tanzania ni moja ya nchi ambazo zimekuwa zikitajwa na mashirika mbali mbali ya kimataifa kuwa ni kitovu cha ujangili wa meno ya tembo katika eneo la Afrika Mashariki.

Hii inatokana na ripoti kadhaa ambazo zinahusu mauaji ya tembo na pembe zake kukamatwa sehemu mbali mbali duniani na pia huko nchini Tanzania. Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari mbali mbali nchini Tanzania, katika kipindi cha Januari na April mwaka huu takriban meno 495 ya tembo yalikamatwa na washukiwa 544 walifikishwa mahakamani katika mikoa mbali mbali nchini humo.

Suala hili limezusha mijadala mikali sana ndani ya nje ya bunge la Tanzania, mijadala yote hiyo ikiishutumu serikali pamoja na idara zinazohusika na hifadhi ya wanyama pori kwa kushindwa kuwalinda tembo wasiendelee kuuawa na majangili.

please wait

No media source currently available

0:00 0:07:00 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mmoja wa wabunge ambaye alivalia njuga suala hili ni Zitto Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini ambaye alisema bungeni kuwa takriban tembo 63 wanauawa kila siku katika hifadhi na mapori ya Tanzania, ikiwa ni zaidi ya tembo 20,000 wanauawa kila mwaka nchini humo. Serikali ya Tanzania imekanusha madai na kusema badala yake kuwa ni tembo 11,000 tu ndiyo huuawa kila mwaka nchini humo.

Kadhia hii ya wizi wa nyara za serikali ni jambo ambalo kwa miaka kadhaa hivi sasa limekuwa likizungumziwa katika kila kikao cha bunge na huwa linatawala mijadala ndani ya bunge wakati wa kujadili bajeti ya wizara inayohusika na maliasili au katika kipindi cha maswali na majibu bungeni.

Mwaka jana kamati ndogo ya bunge inayohusika na ardhi, mazingira na maliasili ilionya kuwa tembo walioko nchini Tanzania watamalizwa katika kipindi cha miaka saba ijayo kama serikali haitachukua hatua madhubuti kulikabili tatizo hili na kuwachukulia hatua wale wanaosadikiwa kuhusika na biashara hii haramu.

Wakati bado ufumbuzi unaendelea kutafutwa ili kuwanusuru tembo na pembe zao kutoweka, utafiti wa taasisi ya elephant trade information system – etis - uliofanywa mwaka jana umebainisha kuwa kati ya mwaka 2000 na 2012 tanzania imeongoza katika usafirishaji haramu wa pembe za ndovu shehena kubwa ya pembe hizo ikifikshwa Hong kong.

Hivi karibuni maafisa wa china walituhumiwa kununua pembe za ndovu kinyume cha sheria. Shutuma hizi za ununuzi haramu wa pembe za ndovu ulitolewa na kampuni ya kimataifa inayojihusisha na masuala ya mazingira ya Environmental Investigation Agency.

XS
SM
MD
LG