Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:21

Wanne wahukumiwa miaka 40 kwa mauaji ya mwanajiolojia.


Mahakama ya Mombasa Kenya.
Mahakama ya Mombasa Kenya.

Mahakama ya Mombasa imewahukumu wanaume wanne raia wa Kenya kifungo cha miaka 40 jela kila mmoja, kwa kuwakuta na hatia ya kumuua mtafiti wa madini raia wa Scotland huko Taveta, karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania.

Watu waliohukumiwa ni Wachimba-migodi huko kwao kaunti ya Taita Taveta, walioshtakiwa miaka mitano iliyopita kwa kumuua Mskochi Campbell Rodney Bridges -mtaalamu wa Madini. Mahakama kuu mjini Mombasa imewahukumu watu hao baada ya ushahidi kuonesha walikuwa na ubaguzi, wakidai kuwa raia wa kigeni alifaidi kutokana na madini fulani yaliyo eneo lao.

Jaji Maureen Odero aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo alisema “Mohamed Dadi, Alfred Njuruka, Samwel Mwachala na James Chacha, walihusika na mauaji ya Campbell Rodney Bridges,raia wa Scotland”. Watuhumiwa walishtakiwa kumuua Bridges raia Agosti mwaka 2009 eneo la Kwambaga Mwasui “Ranch” kaunti ya Taita Taveta.

Mahakama iliwapata na hatia Wachimba-migodi hao, baada ya kusikiliza mashahidi kwa miaka Mitano.

Polisi walikuwa wamewashtaki watu nane lakini wanne wakaachiwa huru, akiwepo mtu aliyetejwa kuwa jamaa wa mbunge wa Taveta Naomi Shaban.

Wakati kesi hiyo ilipokuwa ikisikilizwa Bi. Shaban alimtetea “mjomb wake” kwa kuwasilisha kitabu mahakamani, kuonyesha kwamba alikuwa amemtembelea Nairobi wakati mauaji ya Bridges yaliporipotiwa kutekeelzwa huko Taveta.

Marehemu Bridges Rodney aliishi Kenya kwa Takriban miaka 35, tangu alipozuru mwaka wa 1974, na kusaidia katika utafiti wa madini kaunti ya Taita Taveta.

XS
SM
MD
LG