Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:26

Bunge las Tanzania lina haki kujadili ripoti ya Tegeta Escrow: Ndumbaro


Ndani ya Bunge la Tanzania
Ndani ya Bunge la Tanzania

Bunge la Tanzania limepokea ripoti kuhusiana na kashfa ya Tegeta Escrow, baada ya serikali kujaribu kuzuia suala hilo lisijadiliwe na wabunge. Hata hivyo Spika wa Bunge Bi. Anna Makinda alipinga hoja ya serikali na kueleza kwamba bunge chini ya mamlaka yake linaweza kujadili maswala yanayowasilishwa na wabunge wake.

Mahojiano na Dr Ndumbaro
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:46 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mhadhir wa sheria katika chuo kikuu huria cha Tanzania Dr. Damas Daniel Ndumbaro anasema "Bunge la Tanzania, kwa mujibu wa katiba lina kazi kubwa mbili. Kazi ya kwanza ni kutunga sheria, lakini kazi ya pili ni kusimamia shughuli za serikali, ikiwemu kuikosoa serikali."

Kwa hivyo anasema, kuhusiana na akaunti ya IPTL, ambayo hivi sasa inafahamika kama kashfa ya Tegeta Escrow, ni moja kati ya shughulki za serikali. Kutokana na hayo bunge lina mamlaka kamili ya kulijadili.

XS
SM
MD
LG