Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:22

Ghasia zakumba mji wa Ferguson.


Gari likiungua mtaani baada ya jopo la wateuliwa wa mahakama kutoa uamuzi wa kutomfungulia mashitaka afisa wa polisi aliyemuuwa huyo kijana mweusi. Ferguson, Missouri, Nov. 24, 2014.
Gari likiungua mtaani baada ya jopo la wateuliwa wa mahakama kutoa uamuzi wa kutomfungulia mashitaka afisa wa polisi aliyemuuwa huyo kijana mweusi. Ferguson, Missouri, Nov. 24, 2014.

Jopo lililoteuliwa na mahakama kutoa maamuzi katika jimbo la Missouri nchini Marekani limeamua kutomfungulia mashitaka afisa wa polisi ambaye alimpiga risasi na kumuuwa kijana mweusi asiyekuwa na silaha yapata miezi minne iliyopita.

Baada ya maamuzi hayo kutangazwa, hali katika mji wa Ferguson imekuwa tete huku waandamanaji wakitupia mawe magari ya polisi pamoja na chupa. Polisi nao wanajibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi.

Ghasi hizo zinafuatia tangazo la mwendesha mashitaka wa kitongoji cha Missouri Robert McCulloch Jumatatu usiku kwamba jopo hilo halikuona sababu yoyote ya kumfungulia mashitaka polisi huyo Darren Wilson. Alikuwa afisa wa polisi aliyempiga risasi na kumuuwa kijana Michael Brown Agosti 9, 2014.

Mauaji hayo yalisababisha mvutano mkali kati ya eneo lililo na wakaazi wengi weusi la St. Louis ambalo hufanyiwa doria na polisi,wengi wao wazungu. Uporaji ulitokea usiku baada ya upigaji risasi na maandamano ambayo kwa wakati mwingine yalikuwa ya ghasia kufanywa kwa wiki kadhaa huku polisi wakijibu kwa mabomu ya kutoa machozi.

Baada ya maamuzi kutangazwa Jumatatu usiku familia ya Michael Brown imesema kwamba imesikitika sana. Mawakili wa Darren Wilson wamesema jopo la majaji walioteuliwa limekubaliana kwamba hatua za polisi huyo zilifuata sheria na taratibu za polisi.

XS
SM
MD
LG