Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 21:12

Raia wa India awekwa karantini licha ya kupona Ebola


Msanii wa Indian Sudarshan Pattnaik akitengeneza sanamu kwa kutumia mchanga kutoa ujume wa Ebola.
Msanii wa Indian Sudarshan Pattnaik akitengeneza sanamu kwa kutumia mchanga kutoa ujume wa Ebola.

Raia wa India mwenye umri wa miaka 26 aliyeonyesha dalili za Ebola na kutibiwa akiwa nchini Liberia, amewekewa karantini katika kituo cha uwanja wa ndege New Delhi, nchini India.

Mamlaka za India zinasema mtu huyo alirudi Novemba 10, baada ya kutibiwa Ebola nchini Liberia, na vipimo vya damu kuonyesha hana virusi vya Ebola.

Hata hivyo mamlaka zinasema chembechembe zake bado zinaonyesha dalili za virusi katika vipimo vilivyofanywa nchini India.

Madaktari wansema virusi vya Ebola hubaki mwilini katika majimaji ya mwili hata baada ya kupona na kuhatarisha maambukizi kutokea wakati wa kujamiiana.

India ina takriban raia 45,000 wanao-fanya kazi Afrika Magharibi, na imekuwa ikipima watu wanaowasili kutoka eneo hilo kubaini ikiwa wana virusi hivyo au hawana.

XS
SM
MD
LG