Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:39

Umoja wa Afrika walaani shambulizi la Niger.


walinda amani wa umoja wa mataifa huko Mali
walinda amani wa umoja wa mataifa huko Mali

Umoja wa Afrika umeshutumu vikali shambulizi la walinda amani wa Niger wanaofanya operesheni pamoja na jeshi la la pamoja la kurejesha uthaditi huko mali- au MINUSMA .

Shambulizi hilo limeuwa wanajeshi tisa na wengine kujeruhiwa wakati wa shambulizi la ghafla ijumaa katika taifa hiklo la afrika magharibi kilomita 15 mashariki mwa mji wa Gao nchini humo.

Mwezi uliopita walinda amani wa umoja wa mataifa kutoka Chad walivamiwa na wanamgambo waliokuwa na silaha nchini Mali. Msemaji wa umoja wa afrika , El Ghassim Wane amesema jumuiya ya eneo hilo iko tayari kusaidiana na umoja wa mataifa na washirika wake wa kimataifa kufanya uchunguzi na kuwapata magaidi waliopanga na kufanya mashambulizi. Umoja wa afrika umelaani vikali shambulizi hilo la kigaidi.

Wamesema wako tayari kutoa msaada kwa MINISCA katika utekelezaji wa kazi zake na kutoa wmito kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wote unahitajika kwa MINUSCA.

XS
SM
MD
LG