Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:32

Somalia na Marekani zinathibitisha kuuliwa kiongozi wa al-Shabab


Picha ya Abdi Godane kiongozi wa al-Shabab iliyotolewa kitambo na idara ya ujasusi ya Marekani.
Picha ya Abdi Godane kiongozi wa al-Shabab iliyotolewa kitambo na idara ya ujasusi ya Marekani.

Maafisa wa serikali ya Marekani na Somalia wamethibitisha siku ya Ijuma kwamba, shambulio lililofanywa na ndege isiyo na rubani huko Somalia Jumatatu limesababisha kifo cha Ahmed Abdi Godane, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa kisomali la al-Shabab.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud akithibitisha kuuliwa kwa Godane, katika jimbo la Lower Shabelle, alisema kiongozi huyo wa Al-Shabab aliuliwa pamoja na washauri wake 12 siku ya Jumatatu tarehe 1 Septemba.

Wakati huo huo, kiongozi wa Somali alitoa wito kwa wanachama wote wa al-Shabab kuchukua nafasi hii kujisalimisha na kujiunga na utaratibu wa amani.

Alisema ingawa kutakuwa na wale wenye msimamo mkali kabisa wa kundi hilo watakaopigania uwongozi, lakini alisisitiza kwamba hii ni nafasi kwa wengi wa wanachama kubadili muelekeo wa mambo na kujitenga na uwongozi wa Godane.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mkutano wa viongozi wa NATO huko Wales, Rais Barack Obama amesema, Marekani imekua daima ikifanyakazi kwa makini na mpangilio kumaliza makundi kama hayo ambayo huwenda yakazusha kitosho kwa watumishi wa Marekani au taifa la Marekani.

XS
SM
MD
LG