Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 11:47

Michele Obama awataka wanaume wa Afrika kusaidia kuwawezesha wanawake


Michelle Obama akizungumza katika mkutano wa Viongozi Vijana wa frika - YALI, mjini Washington Julai 30 2014
Michelle Obama akizungumza katika mkutano wa Viongozi Vijana wa frika - YALI, mjini Washington Julai 30 2014

Michelle Obama, mke wa rais wa Marekani amewataka wanaume wa Afrika kuwasaidia wanawake katika vita vya kuleta usawa wa jinsia kote duniani.

Akizungumza katika kikao cha kufunga mkutano mkuu wa kwanza wa mradi wa Mandela kwa ajili ya Viongozi Vijana wa Afrika - YALI mjini Washington, Bi. Obama akishangiriwa na vijana 500 kutoka zaidi ya mataifa 50 ya Afrika, aliwapongeza viongozi hao kwa kazi wanaofanya na kuweza kufika mahala walipo hii leo.

Mke wa rais wa Marekani alisema akiwa Marekani mwenye asili ya kiafrika na kuolewa na Marekani mwenye asili ya Kenya, anafahamu fika safari ndefu wanawake wanapita kuweza kufanikiwa, na kusema "nimefika mahala nilipo kutokana na msaada wa kaka zangu na wanaume katika familia yangu. " alisema Bi. Obama.

Rais Barack Obama akizungumza na vijana wanaohudhuria mkutano wa Viongozi Vijana wa Afrika - Yali, mjini Washington.
Rais Barack Obama akizungumza na vijana wanaohudhuria mkutano wa Viongozi Vijana wa Afrika - Yali, mjini Washington.

Akizungumza kutoka moyoni alisema badala ya watu kuzungumzia rasilmali zinazohitajika kuwezesha ufanisi wa elimu ya wasichana, jambo ambalo bila shaka ni muhimu, lakini amesema inabidi kwanza, watu kuanza kuzungumzia wazi haja ya kubadili tabia, maadili na imani ya jinsi kina baba na kina mama wanavyo wachukulia wasichana wao, kwa kuuliza ikiwa wanastahiki kupata elimu au kuolewa wakiwa wagdogo.

Kutokana na hayo Michelle Obama amewataka vijana walohudhuria wiki sita za masomo na kupata ujuzi hapa Marekani kurudi nyumbani na kuanza kampeni ya kuomngoza miradi ya kuleta mabadiliko bila ya kuwasuiri viongozi wao au serikali zao kuwafanyikia mambo yao.

Vijana wote wameeleza kuridhika na ziara yao na kusema wamepata motisha wa kutosha na wanarudi na nguvu kuweza kuleta mabadiliko barani Afrika.

XS
SM
MD
LG