Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 03:40

Libya yafanya uchaguzi wa bunge.


Wanawake wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura Tripoli, Julai 7, 2012.
Wanawake wakiwa kwenye foleni ya kupiga kura Tripoli, Julai 7, 2012.

Raia wa Libya wanapiga kura Jumatano kuchagua bunge jipya, wakati nchi hiyo ikitaka kumaliza ghasia ambazo zimeendelea tangu kuangushwa kwa kiongozi wa zamani Moamar Gadhafi.

Zaidi ya wagombea 1,600 wanagombea nafasi 200 katika bunge jipya , huku viti 32 vikiwa kwa ajili ya wanawake.


Wabunge hao watachukua nafasi ya bunge lililochaguliwa 2012 na kwamba wengi wanalaumu kukosekana kwa uthabiti ikiwa ni pamoja na mzozo wa kuchaguliwa waziri mkuu mwezi uliopita.

Kiasi cha watu millioni 1.5 wana uhalali wa kupiga kura jumatano , lakini wale walioko mashariki mwa nchi wanaweza kuwa na taabu ya kwenda kupiga kura kwasababu ya ghasia zinazoendelea katika eneo hilo.

Wanamgambo waliosaidia kumwangusha Moamar Gadhafi 2011 bado wako Libya wakitafuta maeneo yao wenyewe na baadhi wakichukua udhibiti wa wa miji muhimu ya bandari jambo ambalo limepelekea kupunguza uwezo wa nchi hiyo kuuza mafuta nje.

XS
SM
MD
LG