Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 01:41

Watu 21 wafariki katika mlipuko wa bomu Nigeria.


Madaktari na wauguzi wakitibu baadhi ya waathirika wa mlipuko wa bomu huko Abuja, Nigeria, Aprili 15, 2014.
Madaktari na wauguzi wakitibu baadhi ya waathirika wa mlipuko wa bomu huko Abuja, Nigeria, Aprili 15, 2014.
Mlipuko wa bomu katika eneo ambalo wapenzi wa mpira Nigeria walikuwa wanaangalia mechi za kombe la dunia umeuwa watu wapatao 21.

Mashahidi na maafisa wa afya walisema Jumatano kwamba watu wapatao 20 wengine walijeruhiwa katika mlipuko huo ambao ulitokea Jumanne katika mji wa kaskazini mashariki wa Damaturu.

Makundi ya watu wengi walikuwa wamekusanyika katika kituo cha eneo la nje cha kuangalia mpira wa kombe la dunia kati ya Brazil na Mexico kwenye televisheni kubwa.
Mashahidi wanasema bomu ambalo inaelekea lilifichwa katika bajaji lilipuka muda mfupi baada ya mechi hiyo kuanza .

Hakukuwa na madai ya mara moja ya kuhusika .Damaturu ni mji mkuu wa jimbo la Yobe na moja ya mikoa ya kaskazini ambayo iko chini ya hali ya hatari, kufuataia mfululizo wa mashambulizi mabaya yanayohusiana na kundi la wanamgambo wa kiislam la Boko Haram.
XS
SM
MD
LG