Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:25

Baraza la usalama laweka vikwazo dhidi ya kundi la Boko Haram.


Mshukiwa wa kundi la Boko Haram, Ali Sanda Umar Kondugaakiwa mahakamani akiwa na seneta Ali Ndume wakati wa kesi yake huko Nigeria November 22, 2011.
Mshukiwa wa kundi la Boko Haram, Ali Sanda Umar Kondugaakiwa mahakamani akiwa na seneta Ali Ndume wakati wa kesi yake huko Nigeria November 22, 2011.
Baraza la usalama la umoja mataifa limeweka vikwazo dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Nigeria Boko Haram, ambalo limefanya wimbi la mashambulizi ya mauaji na hivi karibuni kuteka nyara takriban wasichana mia tatu huko Nigeria.

Nigeria imeliomba baraza hilo kuongeza kundi hilo la wanamgambo katika orodha ya makundi yenye ushirikiano na al qaida, ambayo yamekewa adhabu ya kuzuiwa kwa mali zao, vikwazo vya usafiri na marufuku ya silaha.

Balozi wa Marekani kwenye umoja Mataifa Bi.Samantha Power, alikaribisha hatua hiyo ya baraza, akiita hatua muhimu katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Nigeria kulishinda kundi la Boko Haram na kuwawajibisha viongozi wanaofanya mauaji kwa ukatili waliotenda.

Nchini Nigeria, washambuliaji waliokuwa na silaha waliwauwa takriban watu 29 jumatano jioni katika shambulizi kwenye kijiji cha mbali upande wa Kaskazini mashariki. Hilo lilikuwa shambulizi la tatu kubwa linalolaumiwa kufanywa na Boko Haram wiki hii.

Siku ya alhamisi, walimu kote nchini Nigeria waliingia mitaani kwa maandamano ya siku moja kupinga utekaji nyara wa wasichana wa shule uliofanywa na Boko Haram. Wasichana hao wamepotea kwa zaidi ya mwezi sasa, na nchi kadhaa zimeahidi kuisadia Nigeria katika juhudi zake za kuwatafuta wasichana hao.
XS
SM
MD
LG