Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 10:02

Uganda yapanga kuwarudisha wakimbizi wa Kongo


Wakimbizi wakimbia kutoka Nyabiondo wilayani Masisis DRC
Wakimbizi wakimbia kutoka Nyabiondo wilayani Masisis DRC
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewatolea mwito raia wake wanaoishi Uganda kama wakimbizi waanze kujiandaa kurudi nyumbani kwa sababu usalama umerejea nchini mwao. Wito huu ulitolewa baada ya kumalizika kwa mkutano wa siku tatu siku ya Jumatano terehe 30 April, uliokuwa unafanyika mjini Kampala kujadili njia za kuwarudisha wakimbizi nyumbani mwao.

Maafisa kutoka serikali ya Congo, Uganda na Idara ya Umoja wa Mataifa inayoyashughulikia maslahi ya wakimbizi UNHCR waliamua kukutana na kujadili njia salama za kuwarudisha wakimbizi Wakongomani nyumbani baada ya boti lililokuwa linawabeba wakimbizi waliokuwa wametoroka kwenye kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda kuzama wakiwa safarini kurudi nchini Congo mwezi uliopita.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:27 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Sasa, wakimbizi ambao wanataka kurudi nyumbani kuanzia leo wako huru kuomba msaada kutoka UNHCR warudishwe nyumbani lakini zoezi la kuwarudisha nyumbani litazinduliwa rasmi mwezi wa tisa mwaka huu.

Waziri wa usalama wsa ndani wa DRC, Richard Mangezi, anasema "Serikali za Congo na Uganda pamoja na UNHCR , zitatayarisha mpango wa kuweza kuwarudisha wakimibizi wote nyumbani. wakti huo huo jeshi letu la Congo na wanajeshi wa MONUC wanafanya jitihadi kumaliza hali ya uwasi na ninadhani katika muda wa siku 45 mambo yatakuwa yamekamilika."

Baadhi ya wakongomani niliozungumza nao wanasema hawako tayari kurudi nyumbani.
Serikali ya Uganda imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba kabla ya mwisho wa mwezi wa saba, inafanya utafiti ili kujua kama wakimbizi Wakongomani wanauelewa mchakato huu wa kuwarudisha nyumbani na pia kujua idadi kamili ya wakongomani wanaotaka kurudi nyumbani.

Wakongomani pia watahamasisha kuhusu zoezi hili. Serikali ya Uganda imekaribisha zoezi hili la kuwarudisha Wakongomani nchini mwao. Mapema mwaka huu, Uganda ilianzisha kampeni ya kuchangisha dola milioni 86 za Kimarekani ikisema haikuwa na uwezo tena wa kuwahudumia wakimbizi wote.

Nchini Uganda kuna wakimbizi elfu mia tatu sabini na nne. Congo ndio inayoongoza ikiwa na wakimbizi elfu mia moja themanini na nne. Inafuatwa na Sudan kusini ikiwa na wakimbizi elsfu tisini na tatu. Somalia nayo inashikilia nafasi ya tatu ikiwa na wakimbizi elfu arobaini na moja. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa wizara ya majanga na wakimbizi.
XS
SM
MD
LG