Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 20:55

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa aelekea Moscow na Kyiev.


Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon yuko njiani kuelekea Moscow na Kyiev katika juhudi za kusaidia kutafuta suluhu la kidiplomasia kwa mzozo wa Peninsula ya Crimea.

Ofisi ya Bw.Ban imeeleza kwamba atawasili katika mji mkuu wa Russia Alhamisi na kukutana na rais Vladmir Putin. Na Pia atafanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje Sergei Lavrov na maafisa wengine wa juu .

Ijumaa ataelekea Ukraine ambako atakutana na rais wa mpito Oleksandr Turchymov na waziri mkuu wa muda Arseniy Yatsenyuk na pia maafisa wengine waandamizi.

Msemaji wa Umoja wa mataifa Farhan Haq alirudia kueleza kwamba katibu mkuu alikuwa akitarajia kupatikana suluhisho la kidiplomasia kwa suala hilo.

Siku ya Jumapili eneo la Crimea la Ukraine lilifanya kura ya maoni ya haraka kukiwepo maelfu ya wanajeshi wa Russia na kupiga kura ya kujitenga na Ukraine wakiwa na nia ya kujiunga na muungano wa Russia.Viongozi wa muda wa Ukraine wametangaza kura hiyo ni kinyume cha sheria chini ya katiba ya nchi hiyo.

Wakati wa ziara yake fupi katibu mkuu pia atakutana na wanachama wa tume ya wafuatiliaji wa umoja wa mataifa wakati akiwa Kyiv. Umoja wa mataifa umeomba kupeleka wasimamizi huko Crimea ili kutathmini hali ilivyo.
XS
SM
MD
LG