Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:43

Upinzani Tanzania wataka muswada wa katiba urejeshwe kwa serikali.


Ndani ya Bunge la Tanzania.
Ndani ya Bunge la Tanzania.
Tanzania ikielekea kupata katiba mpya ifikapo mwaka 2014, bunge la nchi hiyo Jumatano limejadili muswada wa sheria ya kura ya maoni wa mwaka 2013 baada ya kusomwa kwa mara ya pili kwenye kamati ya bunge zima.

Akiwasilisha muswada huo bungeni, mjini Dodoma waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Bw. William Lukuvi, alizungumzia namna ya upigaji wa kura hiyo ya maoni ambapo watanznaia ndio watakaoamua kama wanahitaji katiba hiyo kama ambavyo imejadiliwa katika michakato mbalimbali iliyopitia ikiwemo kupitia pia bunge maalum la katiba.

Hata hivyo Kambi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) imeshauri kundolewa kwanza bungeni kwa muswaada huo wa sheria ya kura ya maoni wa mwaka 2013, hadi hapo katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya sasa itakapofanyiwa marekebisho, ili iweze kutambua mchakato wa kura hiyo ya maoni.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo Mbunge wa Singida Mashariki, Bw. Tundu Lissu amesema Katiba ya Zanzibar imeitambua rasmi kura ya maoni na kuiwekea utaratibu katika katiba na sheria yenyewe ya kura ya maoni, kinyume na ilivyo kwa katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania.

Hivi karibuni pia Asasi za kiraia kutoka Tanzania bara na visiwani zilikutana kujadili mchakato wa kuelekea kupata katiba mpya ikiwemo pia upigaji wa kura ya maoni ambapo walisema kwavile tume za uchaguzi za Tanzania bara na Zanzibar bado zina mapungufu kadhaa yanayolalamikiwa, walitaka kuundwa kwa tume huru ya kushughulikia kura za maoni ifikapo wakati wa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, rasimu nyingine ya katiba inatarajiwa kutolewa na tume ya mabadiliko ya katiba baadaye mwezi huu ambapo baada ya hapo rasimu hiyo itajadiliwa katika bunge maalum la katika kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya wananchi.
XS
SM
MD
LG