Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 04:00

Umoja wa Mataifa wapeleka ndege za Drone Congo.


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza na waandishi wa habari.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza na waandishi wa habari.
Umoja wa Mataifa utaanza kurusha ndege zenye kamera zisizotumia rubani-Drones - kwenye anga ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC hapo Jumanne ili kuwasaidia walinda amani kuwasaka waasi na kufuatilia mienendo yao.

Mkuu wa walinda amani katika Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous yupo mjini Goma kushuhudia uzinduzi huo wa Drones. Alisema Jumatatu kwamba hali huko mashariki mwa Congo ni tofauti sana kutoka mwaka mmoja uliopita wakati kundi la waasi wa M23 walipoiteka miji kadhaa katika eneo hilo.

Mwezi uliopita kundi la M23 lilitangaza kuweka chini silaha zake baada ya jeshi la Congo kuteka ngome ya mwisho ya kundi hilo kwa msaada wa kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa.
XS
SM
MD
LG