Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:42

Wamarekani washeherekea Thanksgiving.


Rais Barack Obama, na wanawe Sasha and Malia, wakiadhimisha utamaduni wa Thanksgiving wa kumuokoa bata mzunga aitwaye Popcorn akipata "msamaha wa rais" huko White House Washington, Nov. 27, 2013.
Rais Barack Obama, na wanawe Sasha and Malia, wakiadhimisha utamaduni wa Thanksgiving wa kumuokoa bata mzunga aitwaye Popcorn akipata "msamaha wa rais" huko White House Washington, Nov. 27, 2013.
Kila alhamisi ya mwisho ya mwisho wa Novemba wamarekani hupumzika na kutoa shukran wamarekani wanaadhimisha sherehe ya kila mwaka ya kutoa shukrani kwa yaliowafika kwa mwaka mzima.

Ni utamaduni wa muda mrefu ulioanza tangu kuwasili kwa wakazi wa kwanza wa kiingereza Marekani Kaskazini katika karne ya 17 ambao baada ya mafanikio yao ya kwanza ya mavuno katika ardhi mpya walisimama na kusheherekea mazao yao na kutoa shukrani.
Ikiangukia mwezi wa kipupwe siku ya shukrani ina uhusiano sana na sikukuu za mavuno katika mataifa na utamaduni mbali mbali kama vile maadhimisho ya Trungh Thu huko Vietnam na Homowo, sherehe za kitamaduni za kila mwaka za zao la kiazi kikuu nchini Ghana.

Wamarekani husheherekea Thanksgiving kwa vyakula, kutembelea familia na hapo tena kuanza kwa msimu wa mwisho wa mwaka wa kushushwa bei za bidhaa madukani kabla ya siku kuu ya Krismasi.

Sikukuu hii ni ya kutoa shukran hasa katika sherehe za kifamilia na chakula kikuu ni bata mzinga na vyakula kadhaa vya asili ya Marekani.

Pia gwaride za aina mbali mbali zimefanyika katika takriban katika miji yote ya Marekani na gwaride kuu mashuhuri ni la Macy’s thanksgiving parade huko New York, ambako kulikuwa na hofu ya kuwepo na hali mbaya ya hewa, iliyoharibu safari za wengi kuwasili kwa wakati kwa sherehe zao katika sehemu nyingi za hapa Marekani.
XS
SM
MD
LG