Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 09:59

Kenya yasubiri jibu la Umoja wa Mataifa.


Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Kenya imewasilisha rasmi barua kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuahirisha kesi zinazoendelea katika mahakama ya ICC dhidi ya rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto. Pia, nchi 49 za Umoja wa Afrika zimetia saini barua iliyowasilishwa Jumanne kwa baraza hilo ikiunga mkono kuahirishwa kwa kesi hizo dhidi ya viongozi wa Kenya.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika Jumatano, balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa bw. Macharia Kamau alisema Kenya na Umoja wa Afrika wanasubiri kwa hamu maamuzi ya Baraza hilo.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:57 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika ombi lake Kenya inalitaka Baraza hilo kufikia maamuzi ya haraka kuwawezesha viongozi wake kutohudhuria vikao vya kesi dhidi yao katika mahakama ya The Hague kwa mwaka mmoja.

Balozi Kamau alisema Kenya inakabiliwa na tishio kuu la ugaidi na ukosefu wa usalama hata kutoka pembe ya Afrika. Alisema ombi la Kenya la mwaka wa 2011 katika Baraza hilo halikupata majibu yaliyotegemewa na kwamba viongozi wake bw. Kenyatta na naibu rais Ruto wanahitaji kuwa nchini kusimamia shughuli za usalama na majukumu yao kama wanavyotakiwa na katiba ya nchi hiyo.

Viongozi hao wa Kenya wanakabiliwa na mashtaka mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC kwa tuhuma kwamba walichochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2007 na mapema mwaka wa 2008.

Kesi dhidi ya naibu rais Ruto imekuwa ikiendelea, huku kesi dhidi ya bw. Kenyatta ikitazamiwa kuanza Novemba 12 mwaka huu. Aidha balozi Kamau anasema anatazamia maamuzi ya Baraza hilo yatafikiwa kwa wakati ili rais huyo aweze kupanga mikakati ya ulinzi wa taifa lake ambao ni muhimu sawa na wa nchi nyingine yoyote duniani.
XS
SM
MD
LG