Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 22:01

Wanajeshi saba wa Tanzania waliokufa Darfur waagwa rasmi.

Wanajeshi wa Tanzania waliouwawa Darfur
Wanajeshi wa Tanzania waliouwawa Darfur

Jumuiya ya kimataifa imetakiwa kuangalia upya mfumo wa kulinda amani katika jimbo la Darfus ili kupunguza vifo na majeruhi ya askari wa kulinda amani nchini humo tokea kuanza kwa operesheni ya ulinzi wa amani nchini Sudan.

Akizungumza katika makao makuu ya jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania jijini Dar es salaam wakati wa kuiaga miili ya wanajeshi saba wa Tanzania waliopoteza maisha katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wakiwa kwenye majukumu ya jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa (Unamid), rais Jakaya Kikwete licha ya kukiri kwamba katika ulinzi wa amani masuala ya mauaji na majeruhi hayaepukiki alitaka kuangaliwa upya mfumo wa kujihami kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama katika jimbo la Darfur.

Rais Kikwete pia licha ya kukiri kwamba kuuwawa kwa wanajeshi hao wa Tanzania huko Darfur, kumemsikitisha na kumkasirisha alirudia rai yake kwa Serikali ya Sudan ya kutaka kuchukua hatua dhidi ya mashambulizi hayo.

Kwa upande wake Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa, Shamsi Vuai Nahodha, amesema lengo la waliofanya tukio hilo la kihalifu ni kufifisha juhudi za kusaidia kuleta amani kwenye maeneo yenye migororo lakini hata hivyo amesema hawatafanikiwa.

Askari hao Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo,Private. Rodney Ndunguru, Private. Peter Werema na Private. Fortunatus Msofe walifariki baada ya kushambuliwa na kikundi cha waasi wa Sudani,Julai 13 mwaka huu walipokuwa katika msafara wa kusindikiza waangalizi wa amani kutoka eneo la Khor Abeche kwenda Nyara, katika Jimbo la Darfur.

Tanzania imekuwa nchini Sudan kwa shughuli za kulinda amani tangu mwaka 2007, na Agost 2012 askari wengine watatu Tanzania walikufa maji kwenye mji wa Darfur, Kusini mwa Sudan wakiwa katika Operesheni ya Kulinda amani katika nchi hiyo, baada ya gari lao kusombwa na maji ya Mto Malawasha ulioko katika Kijiji cha Ahamada.

Askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wamekuwa wakishiriki operesheni mbalimbali za kulinda amani za Umoja wa Mataifa na kwa hivi sasa vikosi vya Tanzania viko huko Lebanon, Sudan na Drc.

XS
SM
MD
LG