Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:30

Wafanyakazi Duniani waadhimisha Mayday.



Wafanyakazi duniani kote wanaandamana mitaani Jumatano kuadhimisha siku ya kimataifa ya wafanyakazi duniani ijulikanayo kama Mayday huku wito ukitolewa kwa nyongeza ya mishahara na mazingira bora ya kazi.

Mgomo wa chama cha wafanyakazi Ugiriki siku ya may day umesababisha kadhia ya safari za feri kwenye kisiwa hicho na usafiri wa umma huko Athens ambapo waandamanaji wanaamdamana dhidi ya hatua zilizoongezwa muda za kubana matumizi kiuchumi.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ameahidi kuongeza mishahara ya kima cha chini kwa asilimia 14 na nusu, na kutangaza mikakati mbali mbali ya kuimarisha uchumi wa nchi hiyo katika sherehe za kuadhimisha siku hiyo huko Nairobi.Ifuatayo ripoti ya Mwai Gikonyo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:01 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Na huko Tanzania sherehe hizo ziliadhimishwa mkoani Mbeya na vyama vya wafanyakazi vyataka serikali kuwapunguzia kiwango cha kodi wanachokatwa wafanyakazi.

Akizungumza na Sauti ya Amerika katibu mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi (TUCTA) Bw. Nikolas Mgaya ameitaka serikali kutambua sekta isiyo rasmi kwani ina mchango mkubwa kwa pato la taifa.
Mahojiano na Nicolas Mgaya - 2:34
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wafanyakazi nchi nzima huko Spain ambako ukosefu wa ajira umeongezeka kufikia asilimia 27 wanafanya maanadamano kutaka mabadiliko ya sera za kiuchumi.
Huko Phillippines wafanyakazi wanaandamana huko Manila kudai serikali ilinde ajira zao. Pia wanaidai serikali kuacha kuajiri watumishi wa muda ambao hawapati haki sawa na wale wa kudumu.
XS
SM
MD
LG