Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 00:21

Mbio za Marathon London zafana.


Wakimbia katika mbio za Marathon London.
Wakimbia katika mbio za Marathon London.
Hali ya sherehe ilitaanda katika mbio za marathon za London Jumapili licha ya kuwepo na wasiwasi kufuatia mashambulizi ya bomu wiki iliyopita katika mbio za marathon za Boston nchini Marekani.

Siku sita baada ya mashambulizi hayo karibu na mstari wa kumalizia kwenye mji wa Boston , wakimbiaji huko London walituma ujumbe wenye nguvu wa umoja kwa wakazi wa jimbo wa kaskazinimashariki la Marekani na waathiriwa.

Raia wa Ethiopia Tsegaye Kebede, alishinda mbio za wanaume akimaliza kwa kutumia saa mbili na dakika sita na sekunde nne.

Priscar jeptoo kutoka Kenya aliibuka mshindi katika mbio za wanawake kwa kumaliza mbio za kilomita 45 kwa kutumia saa 2 kadika 20 na sekunde 15.

Takriban wakimbiaji elfu 34 walishiriki mjini London. Waandaaji waliahidi kuchangia dola tatu kwa kila mkimbiaji aliyemaliza, katika fuko la Boston lililoanzishwa kwaajili ya waathiriwa wa mabomu huko Boston.
XS
SM
MD
LG