Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 20:00

Wabunge watimuliwa bungeni Uganda


Bunge la Uganda likiwa katika kikao kamili
Bunge la Uganda likiwa katika kikao kamili
Utata bado unaendelea bungeni nchini Uganda baada ya chama tawala cha National resistance Movement- NRM kuwafukuzwa wabunge wanne kwenye chama hicho.

Katibu mkuu wa NRM Amama Mbabazi alisema wabunge hao baada ya kufukuzwa wamevipoteza viti vyao vya ubunge lakini waathiriwa wanasema hawabanduki bungeni.

Theodore Sekikubo, Mohammed Nsereko, Barnabas Tinkasimire na Wilfred Niwagaba walifukuzwa kutoka chama cha NRM mwishoni mwa wiki kwa kile katibu mkuu wa chama ambaye pia ni waziri mkuu Amama Mbabazi alisema ni upotovu wa nidhamu.
Wabunge wafukuzwa kutoka bunge la Uganda - 2:50
please wait

No media source currently available

0:00 0:02:50 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Waziri mkuu Mbabazi alisema wabunge waliofukuzwa wanatakiwa kuondoka bungeni kwa sababu Kifungu cha 83- G cha katiba ya chama cha NRM kinasema mtu akikiacha chama anakipoteza kiti chake cha ubunge. Mtu kukitafsiri kifungu hiki na kusema unakipoteza kiti unapokiacha chama kwa ihari yako, basi katiba haitafsiriwi hivyo.

Wabunge waliotimuliwa wamesema hawatatoka bungeni kwa sababu katiba ya chama cha NRM inasema wanaofaa kuondoka bungeni ni wale wanaokihama chama kwa hiari yao na sio wale wanaofukuzwa.

Waziri mkuu tayari ameshamwandikia barua spika wa bunge Rebecca Kadaga awatimue kutoka bungeni wabunge waliofukuzwa na NRM. Barua nyingine ikiwa tayari imeshatumwa kwa tume ya uchaguzi kuwafahamisha kuwa waliofukuzwa sio wabunge tena.

Spika wa bunge ambaye anatoka chama cha NRM ni miongoni mwa viongozi wa chama walioketi kwenye kikao kilichoongozwa na rais Museveni kilichoamua ni kina nani waliofaa kufukuzwa kutoka kwenye chama.
XS
SM
MD
LG