Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 07:01

Rai wa Venezuela waomboleza kifo cha Rais wao.


Bendera ya taifa ya Venezuela ikiwa imefunika jeneza la hayati Hugo Chavez.
Bendera ya taifa ya Venezuela ikiwa imefunika jeneza la hayati Hugo Chavez.
Raia wa Venezuela Alhamisi wameingia katika siku nyingine ya kuomboleza kifo cha rais wao Hugo Chaves aliyefariki Jumanne baada ya kuugua ugonjwa wa saratani.

Waombolezaji walijipanga mstari katika kituo cha jeshi cha Caracas ambako mwili wa bwana Chaves umelala kwa ajili ya maombolezo ya kitaifa.

Washirika wa karibu wa bwana Chaves akiwemo rais wa Argentina , Bolivia , na Uruguay tayari wapo Venezuela kwa ajili ya kushiriki kwenye mazishi yake.

Mkuu wa ulinzi wa urais wa Venezuela Jose Ornella, ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba bwana Chaves alikufa kwa shinikizo kubwa la moyo na alikuwa na maumivu makali wakati wa dakika zake za mwisho.

Awali serikali ilithibitisha kwamba bwana Chaves alikuwa na saratani lakini haikufafanua ni ya aina gani.

Jumatano mkusanyiko mkubwa wa raia waombolezaji wa Venezuela walirusha mauwa wakati jeneza la rais huyo likiwasili katika mitaa ya Caracas kutoka hospitali aliyofia akipelekwa katika kituo cha jeshi ambako sasa amelala. Makamu rais mwenye huzuni alitembea kandokando ya gari lililobeba maiti.
XS
SM
MD
LG