Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 21:27

Watalii saba wa Ufaransa watekwa nyara Cameroon.


Rais wa Ufransa Francois Hollande akitoa hotuba huko Paris juu ya operesheni za kijeshi za nchi hiyo.
Rais wa Ufransa Francois Hollande akitoa hotuba huko Paris juu ya operesheni za kijeshi za nchi hiyo.
Watalii saba wa Ufaransa ikiwa ni pamoja na watoto wanne wametekwa nyara huko Cameroon katika kile rais wa Ufaransa Francois Hollande alichokiita ni kundi la kigaidi lenye makao yake Nigeria.

Katika ziara yake huko Ugiriki Jumanne Bw.Holland aliwaaambia waandishi wa habari kuwa anaamini watu wenye silaha walivuka mpaka kutoka Cameroon kuingia Nigeria.

Mateka hao saba ni watu wa familia moja . Shirika la nishati la Ufaransa GDF Suez linasema mmoja wa wafanyakazi wake aliyeko mji mkuu Yaounde alitekwa yeye na familia yake wakati walipokuwa likizoni huko kaskazini mwa Cameroon.

Tukio hilo lilitokea baada ya kundi la kiislam Ansaru kudai kuhusika na kuteka nyara raia saba wa kigeni kaskazini mwa Nigeria
XS
SM
MD
LG