Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 16:22

AU yampongeza Rais wa Madagascar kutogombea kiti cha rais.


Rais wa mpito madagascar Andry Rajoelina.
Rais wa mpito madagascar Andry Rajoelina.
Umoja wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililotolewa na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa hilo kwa miaka kadhaa.

Mwenyekiti wa Umoja huo wa afrika ambaye pia ni rais wa Benin Boni Yayi ametoa pongezi hizo jijini Dar es salama wakati alipokutana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete kujadilia pamoja na mambo mengine migogoro inayoendelea kulikumba bara la afrika na namna ya kusaka ufumbuzi wake.

Kiongozi huyo wa madagasca ametangaza kwamba hatawania kwenye kinyang’anyiro hicho ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwa na majadiliano na viongozi wa sadc waliokutana jijini Dar es salaam kwa ajili ya kusaka suluhu kuhusiana na mzozo wa madaraka uliolikumba taifa hilo tangu mwaka 2009.

Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyoongoza majadiliano ya kupatikana suluhu ya kudumu, amesema kuwa nchi za sadc zimepokea taarifa hiyo kwa furaha kubwa, na akaahidi uungwaji mkono kwa wananchi wa madagasca.

Pamoja na kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Andry Rajolina, kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Umoja huo wa Afrika umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuwafurusha wanamgambo walioliteka eneo la Kaskazini mwa Mali.

Amesema msimamo mkali unaochukuliwa na kundi hilo la wanamgambo ambalo linatajwa kuwa na mafungamano ya karibu ya kundi la alqaida, ni kitisho kwa eneo zima la afrika magharibi hivyo juhudi za pamoja zinapaswa kuchukuliwa sasa ili kuwadhibiti waasi hao.

Zingatio hilo linakuja katika wakati ambapo vikosi vya serikali chini ya msaada wa vikosi vya Ufaransa vikifaulu kuwafurusha wanamgambo hao katika baadhi ya ngome walizokalia, na tayari nchi I wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Afrika Magharibi ECOWAS zimearifu utayari wao wa kuunga mkono operesheni ya kijeshi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kip-moon amepongeza hatua ya uendeshwaji wa opereshni hiyo na ametaka mashirikiano zaidi ili kuwafurusha wanamgambo hao.
XS
SM
MD
LG