Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 21:29

Serikali ya Marekani yaepuka mzozo wa fedha.


Rais Barack Obama akiwa na makamu rais Joe Biden baada ya kutoa taarifa ya muswada kuepuka mzozo wa fedha.
Rais Barack Obama akiwa na makamu rais Joe Biden baada ya kutoa taarifa ya muswada kuepuka mzozo wa fedha.
Shirika la kimataifa la fedha (IMF) linasema hatua za Marekani kuepuka kile kinachoitwa fiscal Cliff yaani kupunguza matumizi ya serikali na kupanda kwa kodi kwa hali ya juu kwa wafanyakazi wa Marekani hazikuzungumzia vya kutosha matatizo ya muda mrefu ya uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na nakisi yake na deni kwa jumla.

Katika taarifa Jumatano jioni msemaji wa IMF Gerry Rice imesema mengi bado yanahitaji kufanywa ili kuweka sawa utaratibu wa fedha wa Marekani kurejea kwenye njia iliyo sahihi bila kuumiza kile kilichotajwa kuwa ni ukuaji tete.

Wabunge wa Marekani katika kikao cha jumanne usiku walipitisha muswada wa kuepuka kile kilichoitwa fiscal cliff yaani kupunguza matumizi ya serikali na kupanda kwa kodi kwa hali ya juu kwa wafanyakazi wa Marekani na mpango ambao rais Barack Obama anauita hatua moja zaidi katika juhudi kubwa za kuimarisha uchumi wa Marekani.
XS
SM
MD
LG